Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia leo limesaini Mkataba wa miaka mitatu wa haki ya Matangaz0 ya TV ya mechi za Ligi ya Championship na Kampuni ya Star Times.
Mkataba huo wa Kihistoria kwa Ligi ya Championship una thamani ya Tsh milioni 613 na utatoa fursa kwa mechi zaidi ya 170 kuonekana Live kwenye TV katika mataifa saba ya Afrika kupitia TV3 (Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji na Afrika Kusini).
‘Tv3 na Tv3 Sports itaanza kuonekana katika muonekano Ang’avu (HD) hivi karibu na kwa Tv3 itakuwa inaonekana kwenye nchi 7 na Afrika Kusini ipo na hapo baada tutaongeza nchi ambazo watakuwa wanaweza kutazama Tv3″- David Malisa Mkuu wa Masoko wa Startimes.
“TV3 kupitia Startimes inaonekana zaidi ya Nchi 7 kote Afrika…Hivyo hii ni fursa kwa wachezaji wetu wa NBC CL kuweza kupata soko katika soka la kulipwa mipaka ya nje ya nchi…”- David Malisa Mkuu wa Masoko wa Startimes.
“Tukio hili ni la kihistoria..Kwa sababu kwa mara ya 2 ndani ya miaka 11 tunaingia mkataba na Televisheni ya nyumbani kuonyesha Ligi yetu ya soka…“- Wallace Karia Rais wa TFF.
‘TV3 itatusaidia kuondoa malalamiko yote ambayo watu walikuwa wanalalamika kwamba walikuwa wanafanyia vitu vibaya na hata wakati mungine wasipofanyiwa vitendo vibaya wanalalamika,kwa hiyo TV3 wataenda kutusaidia”– Wallace Karia Rais wa TFF.
‘Tutakuwa pamoja..uongozi wangu sisi ni waungwana nathamini Tv3 kuja wakati Championship ikiwa katika kipindi kigumu..hivyo mtaendelea kuwa kipaumbele chetu kwa miaka ijayo…baadae mambo yakiwaka’– Wallace Karia Rais wa TFF.
“Najua watu watakuja..lakini sisi tutawapa kipaumbele TV3.Tv3 itafika mbali na Championship itafika mbali pia. Mkataba huu ni wa miaka 3 wenye thamani ya milioni 613 za kitanzania…”- Wallace Karia Rais wa TFF.