Manchester United bado wanaweza kuamua dhidi ya kuamsha chaguo la mwaka mmoja katika kandarasi ya Anthony Martial na kumwachilia Mfaransa huyo kama mchezaji huru mwishoni mwa kampeni.
Martial, 27, amekuwa Old Trafford tangu alipoondoka Monaco mwaka 2015 lakini ameshindwa kutimiza matarajio. Mshambulizi huyo, ambaye amekuwa akikabiliwa na matatizo mengi ya majeraha, ameifungia klabu hiyo mabao 88 lakini alitatizika kuwa fiti wakati Erik ten Hag alipokuwa kocha mkuu.
Na baada ya Mholanzi huyo kutumia pauni milioni 72 kumleta Rasmus Hojlund United kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Martial huenda akakabidhiwa nafasi ya usaidizi msimu huu.
Walakini, ripoti mpya kutoka kwa The Manchester Evening News imeeleza kwamba mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa Martial, ambaye sasa yuko ndani ya mwaka wa mwisho wa mkataba wake ingawa Manchester United wana chaguo la kuongeza mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi, wanaweza kuamua kuachana na Martial msimu ujao wa joto ikiwa hataweza kurejesha kiwango chake.
Ingawa hakuna uwezekano Ten Hag kuchukua uamuzi kama huu katika hatua hii ya mwanzo ya msimu, inabakia kuonekana jinsi uongozi wa Old Trafford ungeitikia iwapo Martial ataondoka katika klabu kama mchezaji huru.
Mmiliki mwenza wa klabu Joel Glazer anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo na hata aliingilia kati kumzuia kocha wa zamani Jose Mourninho asiuze Martial wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Manchester United.