Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema katika mahojiano aliyofanyiwa jana Jumatano kwamba popote ambapo Marekani inatia mkono wake mambo huharibika, usalama unakosekana na mambo yanakuwa magumu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Maria Zakharova, amejibu swali aliloulizwa kuhusu malengo ya kutanuliwa kundi la BRICS kwamba, hatua hizo zinachukuliwa ili kuachana na sarafu ya dola na kuelekea kwenye matumizi ya sarafu za kitaifa ili kuiokoa duniani na majanga yasiyo na mwisho yanayosababishwa na ukiritimba wa sarafu ya dola.
Alisema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la Sputnik na kuongeza kuwa: Mara zote Marekani inapoingilia masuala fulani hufanya mambo kuwa magumu zaidi.
Uhusiano kati ya China na Taiwan ulikuwa umeingia kwenye mkondo mzuri, pande hizo mbili zilikuwa zinaelekea kwenye utulivu kutokana mazungumzo kadhaa ya pande mbili, lakini ghafla moja mambo yamebadilika kutokana na uingiliaji wa Marekani ambao umeharibu kila kitu.
Wakakti huo huo Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza leo Alkhamisi kwamba, imetungua ndege 10 zisizo na rubani za Ukraine kwenye Rasi ya Crimea. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la TASS.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi wa Russia imesema pia kuwa, jeshi la Ukraine limejaribu kushambulia meli ya nchi hiyo katika Bahari Nyeusi kwa kutumia droni lakini zimetunguliwa.
Tazama pia ….