Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mfuko wa Chakula Duniani (WFP) yamesaini makubaliano ya kubadilishana takwimu ili kuboresha misaada ya kibinadamu nchini Somalia.
Makubaliano hayo yatawezesha mashirika hayo mawili kutoa misaada kwa ufanisi zaidi na kwa uwazi kwa watu wenye uhitaji zaidi kwa kuimarisha mikakati na uratibu wa operesheni.
Mwakilishi wa FAO nchini Somalia Etienne Peterschmitt amesema, kwa kubadilishana takwimu, mashirika hayo yanaweza kuwa na ufanisi zaidi kwa rasilimali zao na kuchukua hatua haraka za kuwasaidia jamii zilizo kwenye mgogoro.
Naye mwakilishi wa WFP nchini Somalia El-Khidir Daloum amesema, makubaliano hayo yatasaidia mashirika hayo mawili kutoa misaada ya kuokoa maisha na programu za kubadili maisha kwa jamii nchini Somalia kwa ufanisi zaidi.