Naibu Waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa nishati, Dotto Biteko siku ya leo Sep 14 amefanya ziara fupi kutembelea Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA ikiwa ni mojawapo ya taasisi katika Wizara ya Nishati.
Miongoni mwa mambo aliyoyazungumza Mhe. Biteko ni pamoja ya uwepo wa baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu ndani ya Mamlaka hiyo sambamba na upandaji wa bei ya mafuta nchini.
Aidha Mhe Biteko ameeleza hatua ambazo mpaka sasa Serikali imechukua ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mafuta pamoja na kudhibiti bei ya nishati hiyo.
Tazama zaidi…