Rais Samia Suluhu Hassan amewataka majaji wapya walioapishwa kwenda kuchapa kazi kwa kuzingatia uadilifu, weledi na uaminifu katika maeneo yao ya kazi ili mageuzi yanayotarajiwa na Serikali ndani ya muhimili huo yaonekane.
Rais Samia ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo Alhamisi Septemba 14, 2023 baada kuwaapisha majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, pamoja na viongozi wengine aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ambapo amewataka kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake.
“Kwa Naibu Mwanasheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, sisi Serikali tunasema ndio kitovu chetu, kwa sababu mambo yote yanayotendeka lazima tupate ushauri huko, kama ni kuingia kwenye mikataba ya biasharauwekezaji, kama tumeshtakiwa huko ndiko tunakosimamia mambo yetu yote ya sheria, Kennedy ni Mwanasheria msomi nina imani utakwenda kumsaidia Mwanasheria mkuu kuhakikisha kwamba serikali haingii kwenye matatizo…siku zote anapiga kelele niko under capacity, hawanitoshi sasa tunamsaidia polepole” Mhe.Rais
Aliongeza:”Kwa upande wa Mahakama kuko vizuri, kwa hawa wengine basi nikigundua kuna hivi na vile Zuhura anawahusu na yeye huwa anarusha saa 8 usiku, alfajiri ukiamka hamna kitu, sasa tusifike huko, nendeni kawajibikeni, kila mtu kwa nafasi yake”