Jadon Sancho ameagizwa kufanya mazoezi mbali na kikosi cha kwanza cha Manchester United kwenye “programu ya mazoezi ya kibinafsi” ikisubiri kutatuliwa kwa “suala la nidhamu ya kikosi.”
Hii ilithibitishwa katika taarifa rasmi siku ya Alhamisi.
Meneja wa United Erik ten Hag alimtoa Sancho kwenye kikosi chake cha siku ya mechi kwa ajili ya safari ya kwenda Arsenal mnamo Septemba 3.
Baada ya mechi hiyo Ten Hag alieleza kuwa alichukua uamuzi huo kutokana na tabia mbaya ya mchezaji huyo mazoezini.
Hata hivyo, baadaye siku hiyo hiyo, Sancho aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kudai kwamba amekuwa “azazeli kwa muda mrefu” na kusema madai ya Ten Hag “si ya kweli kabisa.”
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondolewa kwenye mazoezi ya United chini ya Ten Hag, huku winga huyo akifanyiwa programu ya utimamu wa mwili nchini Uholanzi msimu uliopita ambayo ilimshuhudia akitazama Kombe la Dunia kwa mbali.