Rais Samia leo ameanza ziara ya siku tano katika mikoa ya Mtwara na Lindi, ambako na kukagua miradi ikiwamo hospitali, bandari, kiwanja cha ndege, chujio la maji na barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ahmed Abbas amesema ziara ya Rais Samia italeta hamasa kwa wananchi hivyo kukuza uchumi.
Abbas alisema wananchi wa Mtwara wanajivunia kutembelewa na Rais Samia na anaamini kiongozi huyo ataacha alama kwa wananchi katika mkoa huo.
Pia rais Samia Suluhu amezinduana kuweka jiwe la msingi kwenye hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini iliyogharimu Sh bilioni saba huku ujenzi wa hospitali hiyo inayotarajiwa kuhudumia wakazi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma umegharimu Sh bilioni 15.8.
Wananchi wa mkoa wa mtwara pia wameishukuru serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwepo wa hospitali ya rufaa kanda ya kusini mkoani humo.