Benki ya NMB imefungua rasmi mwaka wa pili wa ufadhili wa masomo na usimamizi wa 2023/2024 kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini,kupitia programu ya NMB NURU YANGU scholarship and mentorship,ambako itafadhili wanachuo 65 kwa kiasi cha Sh.Bilioni 1 zinazojumuisha ufadhili wa wateule wa Mwaka wa kwanza.
Ufadhili huo unatolewa kupitia asasi ya kiraia ya NMB Foundation ambayo inajikita katika kusimamia na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika sekta za Kilimo,Elimu,Afya,Mazingira na Ujasiriamali ambapo mwaka jana ilifadhili wanafunzi 65 ambao wanaendelea na masomo katika vyuo vikuu mbalimbali.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo unaoanza Septemba 15 hadi Oktoba 8,Meneja Mkuu wa NMB Foundation,Nelson Karumuna,alizitaja sifa za waombaji kuwa ni ufaulu wa kidato cha sita kwa daraja la kwanza pointi 3 hadi daraja la kwanza pointi 7,na lazıma awe ametoka kwenye mazingira magumu yenye changamoto.
Ufadhili huo ambao unaenda katika maneneo ya ada,posho,stationary,mafunzo ya kompyuta mpakato(laptop),unatolewa kwa wanachuo wa fani za Hesabu na Takwimu,Biashara,Uchumi,Teknolojia,Habari na Mawasiliano,Uhasibu,uhandisi pamoja na Udakatri.
Aliongeza kwa kusema “mwaka huu tutafadhili wanafunzi 65,hivyo kuifanya NMB Foundation uwa na wanafunzi 130 hadi mwaka wa masomo wa 2023/2024 utakapoanza”.
Programu hii pia inatoa usimamizi maalum ‘mentorship’ kuwawezesha kupata ushauri, na pia tukitarajia kuibua vipaji na kuwasaidia vijana hao kutimiza ndoto zao kielimu.