Mwimbaji na mtunzi maarufu wa Nigeria, Teniola Apata anayejulikana kama Teni alijitokeza hadharani kufichua anachotaka watu waandike kwenye kaburi lake atakapofariki.
Akiongea kwenye kipindi cha “Tea with Tay Podcast”, Teni alifichua kuwa kwenye kaburi lake, anataka waandike kuwa aliishi maisha yake kwa matakwa yake mwenyewe. “Case crooner” aliendelea zaidi kufichua kwamba anataka kufa akiwa na furaha.
Kwa maneno yake yalikuwa hivi…
“Kwenye kaburi langu nataka waandike ‘She lived life on her own terms’, ndio natamani kufa na furaha, nitakufa tu.
‘Watu wengi wamebeba ukuu ndani yao lakini wanaogopa sana. kujieleza. Niamini, uwanja wa makaburi umejaa ndoto na vipaji vingi, vitu ambavyo vingeweza kubadilisha ulimwengu”.
“Na unaona kuogopa watu watasema nini, watu hawataacha kuongea naapa kwa Mungu.Kuna watu niliowafanyia wema wananichukia, kuna watu nimewasaidia mtatoka nje watanisema vibaya. Haijalishi utafanya nini, watakuwa mtu ambaye hatapenda unachofanya.”
“Siishi maisha yangu kwa kuomba ukubali kwako, kikubwa kukubalika ni mimi kujikubali, chochote nje ya hapo, siwezi kukusaidia samahani, nitakuwa mwenyewe kwa kila njia. “,
Teni alisema na kuibua hisia kubwa kutoka kwa umma kwa ujumla.