Kamishna wa Polisi wa kamisheni ya Utawala na manejimenti ya rasilimali watu CP Suzan Kaganda leo septemba 20, 2023 amewasilisha taarifa ya Mkutano wa Jumuiya ya Polisi wa kike ukanda wa Afrika IAWP Afrika chapter uliyofanyika mwishoni mwa mwezi Julai,za 2023 jijini Dar es salaam, katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya askari Polisi wa kike Duniani IWAP unaoendelea Auckland New Zealand.
CP Suzan Kaganda amewasilisha taarifa hiyo katika Mkuu wa IWAP ambao umehudhuriwa na nchi (65) yakiwemo mataifa mengine ya Afrika ambayo ni Tanzania, Afrika kusini na Ghana ambapo kimefanyika kikao cha wanachama wa kudumu wa Jumuiya hiyo Annual General Meeting (AGM) ya IAWP, Tanzania ikiwa kanda ya 21 ya nchi ya SADC na mjumbe aliyechaguliwa kwa kanda hiyo ni kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala kamishna msaidizi wa Polisi ACP Dr. Debora Magiligimba kutoka Tanzania.
Aidha kamishna Kaganda ametumia fulsa hiyo kuwakaribisha wajumbe wa Mkutano wa IAWP Tanzania ambapo nchi hiyo inategemea kuwa mwenyeji wa mkutano wa IAWP 2024 huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya ,muungano wa Tanzania na amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kufanya Mkutano huo hapo mwakani kauli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka kwa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi mapema mwezi huu katika bwalo la maafisa wa Polisi jijini Dar es salaam.
Pia washiriki wa Mkutano huo kutoka Tanzania walipata fulsa ya kukutana na Balozi Baraka Luvanda wa Tanzania Nchi Japan ambaye anasimamia Nchi ya Australia na New Zealand Katika kikao hicho na Profesa Ernest Mudogo ambapo Kamishna Kaganda alimuomba Balozi huyo kupitia ubalozi wake kulisaidia Jeshi la Polisi Tanzania katika kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa na askari wa vyeo mbalimbali katika mataifa hayo ya Nje ili kubadilisha uzoefu na mafunzo ambayo yataleta ufanisi katika kazi za Jeshi hilo.
Sambamba na hilo Profesa Ernest Mudogo ambaye ni Diaspora New Zealand amewambia wajumbe kuwa ataendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuleta matokeo Chanya ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi nchini Tanzania,nao baaadhi ya maofisa waliopata fulsa ya kuchangia katika kikao hicho ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala ACP Debora Magiligimba ambae alisisitiza kushirikiana katika mafunzo na nchi hizo ambazo zimeendelea katika Teknolojia na mafunzo ili kuleta ufanisi wa kazi za Polisi nchini Tanzania.
Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi alishauri kushirikiana katika kuboresha maabara za kiuchunguzi wa kisayansi huku akibanisha kuwa kwa kufanya ivyo kutaleta matokea Chanya na kupunguza malalamiko kwa wananchi pale kesi zinapotegemea Ushahidi wa kisayansi.
Pia Mrakibu wa Polisi SP Fatuma Kigondo alisema kuwa mahusiano baina ya Jeshi hilo na Balozi hizo yanapaswa kuendelea ili kujenga mawasiliano na nchi husika katika kuleta mabadiliko na mashirikiano na Majeshi ya Polisi na nchi nyingne za Afrika na ulaya.