Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amehotubia mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kuishtumu Urusi kwa kuendeleza vita katika nchi yake na kuwateka watoto, jambo ambalo ameliezea kama mauaji ya kimbari.
Volodymyr Zelensky amekuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kuzungumza katika mkutano huu maalum, ambapo zaidi ya viongozi sitini wamepangwa kutoa hotuba zao chini ya uenyekiti wa Albania
Hii ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini mwake, Februari 24, 2022, kwa rais Zelensky kuzungumza ana kwa ana mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
“Tunajaribu kuwarejesha nyumbani watoto ila muda inakwenda sana, nini kitatokea? hao watoto walioko kule Urusi wanaichukia Ukraine na uhusiano wowote wa familia zao umevunjika.” amesema rais Zelensky.
Rais wa Marekani Joe Biden, naye pia amelaani vita vinavyoendelea na kuitaka Urusi kusitisha vita.
Kauli hii inakuja wakati huu viongozi wa dunia wakionekana kugawanyika kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine.
“Urusi peke yake inawajibika kwenye vita hivi, Urusi pia inauwezo wa kumaliza vita hivi na ndio nchi pake inasimama kinyume na kumaliza vita hivi kwa sababu madai ya Urusi ya amani ni hasara kwa Ukraine.” amesema rais Joe Biden.