Wagombea wawili wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Februari, wamewasilisha kesi katika mahakama ya upeo kupinga hatua ya kutupiliwa mbali kwa kesi yao dhidi ya ushindi wa rais Bola Ahmed.
Kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa na Peter Obi wa chama cha Leba na mwenzake Atiku Abubakar wa chama cha PDP ilitupiliwa mbali mwezi jana kwa misingi kuwa hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuunga mkono madai yao.
Katika uamuzi wao, majaji waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo walisema viongozi hao hawakuwa na uwezo wa kutihibitisha kwamba uchaguzi huo wa mwezi Februari ulikuwa na kasoro.
Atiku Abubakar anataka mahakama ya upeo kubatilisha uamuzi huo wa awali kwa misingi kuwa hakufuata sheria kabla ya kuidhinisha ushindi wa rais Tinubu.
Kwa upande wake Peter Obi anaithumu mahakama kwa kutozingatia masuala ya umuhimu kuhusu madai yake na kesi aliyowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu mwa mwezi Februari. Hakuna tarehe iliyotolewa ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.