Mfalme wa Uingereza Charles III anatazamiwa kuanza leo, ziara ya siku tatu nchini Ufaransa, miezi kadhaa baada ya ziara hiyo kuahirishwa kutokana na maandamano yaliyokuwa yakiendelea nchini humo.
Mfalme wa Charles wa tatu ,pamoja na mkewe, malikia Camilla watawasili Paris miezi sita baada ya ziara hiyo kulazimika kuahirishwa kufuatia maandamano ya kupinga mfumo wa pensheni, yaliyoshuhudiwa nchini humo kwa muda.
Katika ratiba maalum, mfalme na mkewe watashiriki chakula cha jioni katika kasri ya Versailles .
Mfalme Charles anatazamiwa vile vile kuhutubia bunge la Senate ,hotuba ambayo huenda atatoa kwa lugha ya kifaransa.
Kuna pia mikutano ya wanajamii, wanamichezo kisha ziara kusini Magharibi mwa Ufaransa eneo la Bordeaix ambalo kwa wakati mmoja lilitawaliwa na familia ya Charles na ambapo pia ni makao ya raia wa Uingereza karibu elfu 40.