Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) Jumanne imefichua kisa cha udukuzi, tukio la kihalifu katika moja ya taasisi zenye hadhi ya juu duniani.
Mahakama ya ICC ilisema iligundua shughuli zisizo za kawaida kwenye mtandao wake wa kompyuta mwishoni mwa wiki iliyopita, na kusababisha jibu ambalo bado linaendelea.
Msemaji wa mahakama hiyo amekataa kutoa maelezo juu ya ukubwa wa udukuzi huo, na iwapo tatizo hilo limemalizika kabisa au nani alifanya udukuzi huo.
“Hatua za haraka zilichukuliwa kukabiliana na tukio hilo la udukuzi wa mtandaoni na kupunguza athari zake,” ICC imesema katika taarifa.
Mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita yenye makao yake the Hague Uholanzi, iliundwa mwaka 2002 kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Waendesha mashtaka kwenye mahakama hiyo kwa sasa wanafanya uchunguzi wa kesi 17 kuhusu Ukraine, Uganda, Venezuela, Aghanistan na Ufilipino kati ya nyingine.