Mahakama nchini Nigeria imewaachia kwa dhamana watu 69 waliokamatwa mwezi uliopita wakati wa oparesheni katika kile maofisa wa polisi kwenye taifa hilo walisema walikuwa wanahudhuria sherehe ya harusi ya wapenzi wa jinsia moja.
Suala la mapenzi ya jinsia moja linatajwa kama uovu nchini Nigeria sawa na baadhi ya mataifa mengine ya bara Afrika.
Nigeria inasheria kali kuhusu suala hilo la mapenzi na ndoa ya jinsia moja.
Wakili wa washukiwa hao 69, amesema wateja wake wataachiwa huru kwa dhamana baada ya kuwasilisha dhamana ya zaidi ya dolla mia sita kwa mahakama.
Polisi walitekeleza oparesheni katika hoteli moja katika eneo la Warri baada ya kupokea taarifa kutoka kwa umma kuhusu shughuli ya harusi ya wapenzi wa jinsia moja.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, liliwakashifu polisi nchini Nigeria kwa kuwatangaza wazi kwenye vyombo vya habari washukiwa hao na kuwauliza maswali kuhusiana na tuhuma walizokuwa wanakabiliwa nazo.