Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Shamata Khamis amesema Teknolojia ya nyasi za Juncao ni suluhisho la mgogoro kati ya wakulima na wafugaji sambamba na kutoa fursa ya ajira nchini.
Waziri Khamis amesema nyasi hizo zitapunguza umaskini na kukuza pato la Taifa kupitia sekta kilimo na ufugaji kwa sababu nyasi za Juncao zitatumika katika malisho ya wanyama mbalimbali.
“Tafiti zinaonesha teknolojia hiyo itapunguza vifo vya mifugo na kuleta uhakika wa chakula Duniani ifikapo 2030,”
Kwa upande wake Mhadhiri na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA Dr.Elly Ligate, amesema nyasi hizo pia zinatumika kuzalisha uyoga ambao ni chakula na dawa Kwa binadamu lakini pia zinatunza mazingira Kwa ardhi inayo momonyoka.