Mfalme Charles III na Malkia Camilla wanaanza siku ya pili ya ziara yao ya serikali ya Ufaransa baada ya karamu ya kifahari na wageni 160, akiwemo Mick Jagger, mfalme atahutubia seneti leo kwa mara ya kwanza kihistoria.
Washiriki wa familia ya kifalme, ambao walikuwa wageni wa heshima, waliandamana na Rais Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron Jumatano jioni kwenye ukumbi wa Vioo wa Jumba la Versailles.
Mfalme na Bw Macron walihutubia safu ya nyota wa Uingereza na Ufaransa, akiwemo Hugh Grant, Mick Jagger, Arsene Wenger na Didier Drogba.
Mfalme alizungumza kwa hisia kuhusu uhusiano wa mama yake na Ufaransa alipokuwa akielezea juu ya “urafiki thabiti” kati ya mataifa kwenye karamu ya serikali huko Paris.
Wageni 160 walikula kamba, kuku wa Bresse na jibini.
Leo, Charles atakutana na wawakilishi kutoka kwa Seneti na Bunge la Kitaifa katika Mikutano ya Salle des ambapo atatoa hotuba yake, akiweka historia ya kuwa mfalme wa kwanza kabisa wa Uingereza kuhutubia seneti.
Charles na Camilla kisha watakutana na nyota wa michezo na vijana walio katika mazingira magumu huko Saint-Denis, ambapo Ufaransa itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Raga kabla ya kutembelea Kanisa la Notre Dame Cathedral lililoharibiwa na moto na soko la maua la Paris.