Mpinzani na mkosoaji mkubwa wa Ali Bongo, rais aliyepinduliwa madarakani chini Gabon, Jean Ping amekutana na kiongozi wa nchi hiyo aliyechukuwa mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema huku hali ya utulivu ya kisiasa ikiendelea tangu Agosti 30.
Mkutano huo ulifanyika kwa awamu mbili. Kwanza kati ya Jean Ping, wasaidizi wake na rais wa mpito Brice Clotaire Oligui Nguema akiwa na wajumbe wa baraza lake la mawaziri.
Jean Ping na kiongozi mpya wa Gabon Brice Clotaire Oligui Nguema walikutana ana kwa ana kwa mazungumzon na mwishoni mwa mazungumzo yao, Jean Ping, mwenye aliondoka huku akitabasamu, na kubadilisha msimamo papo hapo.
“Nimepewa heshima yangu kama mmoja wa watu muhimu katika nchi hii na nimefurahi kuwa na mazungumzo na kiongozi mpya nafikiri narudia tena kwamba rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Brice Oligui Nguema, amefanya kazi kubwa ya kusafisha nchi.
Kila mtu anamtambua, kila mtu anampenda na sisi tupo, tayari kufanya kazi, tayari kufanya naye kazi na tayari kuchukua majukumu yetu, ikiwa tutaombwa tuyachukue tunavyoamini! ”
Kwa miaka saba iliyopita, Jean Ping ameishi katika kifungo cha nyumbani katika makazi yake katika eneo la Charbonnages. Amekuwa akiendelea kudai ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 ambao anaamini kuwa uliibiwa na Ali Bongo.