Patric Kimaro maarufu kwa jina la Sabasita Mkazi wa Kata ya Masama katika katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Askari Mstaafu aliyehudumu ndani ya Jeshi la Polisi kwa miaka 36 kwenye mahojiano maalumu na Ayo TV amesema ameshaandaa kaburi lake pamoja na kujichongea jeneza lake huku vitu vyote vikigharimu shilingi million 10.
Sabasita amesema atafariki kwa kifo ambacho mwili wake hautaonekana na yatachukuliwa mabaki kwa ajili ya kuzikwa lakini kama Familia au Mtu yeyote atakiuka na kumzika sehemu nyingine atapata shida ikiwemo kutokewa na kidudu Mtu ambaye atamsumbua.
Askari huyo aliyestaafu amejenga kaburi hilo huku akisema sababu ni kutaka Familia yake isihangaike katika mazishi yake lakini pia alianza kujenga na kuandaa baadhi ya vitu vya mazishi yake kidogokidgo kwa miaka miwili.