Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amewataka Wafanyabiashara na wazalishaji kuacha visingizio vya kudai kuwa mfumo unasumbua unapofika wakati wa kulipa kodi huku kusema itafanyika operesheni maalumu ya ukaguzi wa wafanyabiashara wasiotumia EFD mashine ili kutambua wakwepa kodi na wanaosababisha serikali kukosa mapato.
Malima ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu cha wafanyabishara na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro ambapo amesema amebaini kuwepo kwa kundi la wafanyabishara wakwepa kodi ambapo hawatoa risiti kwa makusudi kwa kisingizio cha mtandao.
RC Malima amesema kufanya hivyo ni makosa kisheria kwani ni kuinyima serikali mapato ambapo amesema siku isiyo na jina watafanya operetion kwa wafanyabishara ili kuwabaini ambapo wamekua wakikataa kutoa risiti kwa makusudi..”kuna siku nimeenda kuweka mafuta nikaulizwa mzee utanataka risiti nikajibu ndio wakasema mfumo haufanyi kazi sasa hii haikubaliki kuna mchezo unafanywa na hawa wafanyabishara”
Kwa upande wake Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Chacha Gotora amesema kikao hicho kitaleta tija kwani wamepata fursa ya kuzungumza na wafanyabaishara pamoja kushaurina masuala ya ulipaji kodi.
Anasema TRA imekua na mfumo wa kutoa elimu mara kwa mara kwa wafanyabishara wadogo na wakubwa lengo kuondoa changanmoto ambazo zimekua zikijitokeza kati ya pande hizo mbili ili kuborehs utendaji kazi.
Naye mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara (TCCIA) Mkoa wa Morogoro Mwadhini Myanza amewasisitiza wauzaji na wanunuaji kuwa makini na majina yanayoandikwa kwenye risiti pamoja na kuchukua risiti zao kwani zinaweza kutumika vibaya.
Mwadhini amesema elimu waliyoipata wataenda kuwapatiwa wafanyabisara wa vijijini ili nao wapate fursa ya kutambua masuala mbalimbali ya kikodi wanayowakabili ikiwemo changamoto ya mfumo katika utoaji risiti.