Klabu ya Simba SC kupitia kwa Meneja wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ahmed Ally imetoa taarifa rasmi kuhusiana na Beki wao wa kimataifa wa Cameroon Che Malone Fondoh kuwa amepata ajali.
Simba SC wamesema ni kweli Che Malone alipata ajali usiku wa kuamkia leo akitokea Airport kuwapokea Ndugu zake lakini yupo sawa hajaumia na kesho ataendelea na mazoezi.
“Ni kweli Che Malone Fondoh amepata ajali usiku wa kuamkia leo akitokea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ambapo alikwenda kuwapokea Ndugu zake kuna Kaka zake wamekuja hapa Tanzania”
“Wakati anarejea kurudi nyumbani kwao maeneo ya Mbezi kufika Mikocheni ndipo ambapo akapata ajali taarifa inaeleza alikuwa akimkwepa Mwendesha pikipiki akaingia mtaroni lakini walikuwa wanne Kaka yake ameumia kidogo ametibiwa na kurejea nyumbani”