Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi, amekanusha uvumi kuhusu mapinduzi nchini mwake alipokuwa ziarani katika mataifa ya kigeni kwa muda wa wiki mbili.
Rais Ndayishimiye amekuwa nchini Cuba kwa ziara na kuzuru pia kule nchini Marekani ambako alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Siku moja baada ya kiongozi huyo wa nchi kuondoka nchini mwake tarehe 10 ya mwezi Septemba, taarifa ziliaanza kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwepo kwa njama ya kutekelezwa kwa mapinduzi dhidi yake.
Katika hotuba yake alipofika nchini Jumanne, Rais Ndayishimiye alisema: “Unaona wanasema ‘Waburundi huacha kulima lakini hawaachi kuongea’, ambapo wanaweza kusema naweza kuwazuia kufanya kazi na wote wanakaa kwenye uvumi , halafu mnakaa na kuwapiga uvumi, kisha wanaacha kufanya kazi na kufa njaa hadi kesho.
Ndayimyimiye alisema kuwa uvumi huu uliletwa na wale ambao siku zote wanataka “kuichafua Burundi kwa sababu wanaona ina sauti tena duniani”.
Alisema, “Kwa hiyo hao ndio utawakuta wakisema ‘kwa hiyo tufanye nini? Nitaudanganya walimwengu yale ambayo huwa tunawadanganya hata kama ni uongo kwao, tuwavunje mioyo watu wa Burundi.”