Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema jeshi lake limepokea vifaru vya kivita aina ya Abrams kutoka nchini Marekani, hatua anayosema imepiga jeki vikosi vya jeshi la Kyiv katika vita vyake dhidi ya wanajeshi wa Urusi.
Kyiv ilitangaza mwezi Juni kuaanza mashambulio ya kuwaondoa wanajeshi wa Urusi katika ardhi yake na imekuwa ikipokea baadhi ya silaha ya kivita kutoka kwa washirika wake nchi za Magharibi.
Akithibitisha kuwasili kwa vifaru hivyo kwenye mtandao wa kijamii, rais Zelensky hakuweka wazi ni vifaru vingapi vimepokelewa na wanajeshi wake na namna vitatumika katika uwanja wa kivita.
Washington ilikuwa imeahidi kuihami Kyiv na vifaru 31 aina ya Abrams kuaanzia mwanzoni mwa mwaka huu, hii ikiwa ni sehemu ya mpango wa msaada wa Dola bilioni 43 wa usalama kutoka kwa Marekani katika kipindi cha miezi 18 iliyoipta.
Hatua ya kuihami Ukraine na vifaru aina ya iliafikiwa tena baada ya awali wizara ya ulinzi ya Marekani kusema uwezo wake ulikuwa mkubwa kwa maofisa wa jeshi la Ukarine.