Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania, limewaomba wadau kuchangia ujenzi wa makao makuu yake yaliyopo maeneo ya Kivule, jijini Dar es Salaam.
Ombi hilo limetolewa katika harambee ya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi wa jengo la makao makuu ya baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika harambee hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mayasa Sadala, alisema ili wamepanga kujenga jengo lenye ghorofa Tano, lakini wamekwama kutokana na ukata wa fedha.
“Kuna eneo tumepanga kulinunua lakini hatujamaliza fedha tumelipa milioni 40, bado milioni 10 hivyo tunaomba wadau watuunge mkono kumaliza pamoja na kupata fedha za ujenzi wa makao makuu yetu,” ameswma Sadala.
Katika Harambe hiyo, wadau mbalimbali walitoa michango Yao kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa eneo la mikutano unagharimu Sh. 6,000,000.
Miongoni mwa wadau hao ni mwanajamii Bihimba Mpaya, aliyetoa matofali 1,000 yanayogharimu zaidi ya Sh. 1,000,000 na mabati matatu.
“Katibu wenu alinipa mualiko wa kuhudhuria harambee, nilikubali japokuwa Sina kitu lakini Mungu amenipa nguvu na sina mali nyingi bali nina moyo wa kutoa. Leo nimekuja na sadala yangu tofsli 1,000,” amesema Mpaya na kuongeza:
“Na mimi sitoi misaada kwa waislamu wenzangu tu bali kwa jamii nzima sababu napenda maendeleo ya watu.”
Katika hatua nyingine Amirati wa Wilaya ya Temeke, Sumaiya Abdallah, amewashukuru wadau wote waliotoa michango Yao.