Uzinduzi wa msaidizi wa kidigitali (chatbot) anayejulikana kama Kai, umeletwa rasmi kubadilisha mfumo mzima wa utoaji wa huduma za kibenki huku hatua hii muhimu ikizidi kuthibitisha malengo ya benki katika kutoa huduma zenye lengo la kumridhisha mteja kwa kiasi kikubwa.
Tangazo hili lilifanyika katika webinar amabyo iliandaliwa maalum na benki ya Stanbic Tanzania kujadili maendeleo yaliyopatikana kupitia sekta ya kidigitali, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency .
Kai, msaidizi huyu mwenye weledi wa hali ya juu, analeta mapinduzi katika jinsi wateja watakavyokuwa wakipata taarifa na msaada wa kibenki,anakuja kurahisisha, kuharakisha na kuhakikisha huduma za kibenki zinapatikana kwa uhakika.
Mkuu wa kitengo ya Biashara wa Stanbic Bank Tanzania, Fredrick Max, alisema, “Tunayo furaha kumtambulisha Kai, ambayo ni hatua kubwa sana katika safari yetu ya mapinduzi yetu ya kidigitali. Kai ataongeza kasi yetu katika kuwahudumia wateja wetu wanaojumuisha Wafanyabiashara Wadogo na Kati (SME) na kuthibitisha kwa mifano ni jinsi gani tumejikita katika kutimiza mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku kwa kuwapatia huduma ambazo si tu zainapatikana muda wote, bali pia zinapatikana kwa ubora wa hali ya juu.
Zaidi ya hapo, Kai anaendana na malengo ya kibiashara na yanayolenga kumridhisha mteja ya benki ya Stanbic hasa kuelekea katika ufanisi na upatikanaji zaidi wa huduma zake. Ubunifu huu hauongezi tu ufanisi katika utendaji wa ndani, lakini pia unonyesha jitihada za benki katika kuwa kinara wa teknolojia katika huduma za kibenki.
“Kwa wateja, Kai anaonyesha ni jinsi gani watahudumiwa katika ubora wa hali ya juu. Tumejikita katika kuwapatia msaada na nyenzo wanazohitaji katika kufikia malengo yao ya kifedha bila usumbufu. Uzinduzi wa Kai unatuwezesha kukidhi mahitaji yao yanayobadilika kila siku kwa kuwapatia msaada wa haraka na rahisi katika kufikia akaunti zao na kufanya miamala” Aliongeza Max.