Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo September 26,2023 amewaapisha Viongozi mbalimbali Wateule Ikulu jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema amelazimika kumhamisha Maharage Chande kutoka TTCL kwasababu amegundua ana Kampuni inayaofanya kazi ndani ya TTCL.
“Maharage tumekutoa TANESCO na nikachukulia uzoefu wako kwenye DSTV n.k, nikaona TTCL ingekufaa zaidi, sasa baadaye nikagundua una biashara ndani ya TTCL na kwasababu Kampuni ile inafanya vizuri na ndio maana imemuwezesha Kijana yule nae kufanya vizuri nikasema hapana usiende mahali ambako una biashara itakuwa conflict of interest”
“Nikaona sasa nikupe Upostamasta Mkuu, mwezi uliopita nilishiriki mkutano wa Posta Afrika pale Arusha, nikakuta Posta yetu wanakwenda kidigitali nikajua hayo ni maeneo yako”
“Na Postamasta wetu amekwenda mafunzo, yupo kwenye mafunzo akirudi tutampangia kazi nyingine, kwahiyo nikaona kwasababu ni maeneo yako na nimemkuta Kijana mzuri sana wa lile eneo la Posta kidigitali kwahiyo nikajua nyie wawili mtakwenda vizuri, nenda kamsaidie mukuze Posta yetu iende kidigitali”