Waziri wa katiba na sheria Pindi Chana amepongeza ofisi ya wakili mkuu wa serikali mkoani hapa pamoja na ofisi zake ambapo Katika kipindi cha miezi 9 ofisi ya wakili mkuu wa serikali pamoja na ofisi za mashtaka zimeokoa zaidi ya bilioni 6 kwa kuisemea serikali.
Ni katika ziara zake waziri wa katiba na sheria Pindi Chana za Kupokea taarifa katika ofisi za mashtaka mkoani Iringa na ofisi ya wakili mkuu wa serikali na ikiwa ni sehemu ya ziara zake katika ofisi zote zinazosimamiwa chini ya wizara ya katiba na sheria
Chana amebainisha kuwa katika mashauri ambayo serikali imeshindwa kwasasa hakuna na mashauri matano yameisha kwa njia ya usuluhishi pamoja na uwepo wa wakili wa serikali na mashauri manne yaliondolewa mahakamani.
Hatahivyo mkuu wa mashtaka mkoa wa Iringa Basilius Namkambe amesema kwasasa mkoa wa Iringa msongamano katika magereza umepungua na wafungwa ni wengi kuliko mahabusu.