Taasisi isiyo ya kiserekali yenye makao makuu nchini Norway, Stromme foundation, imekutana na wadau mbalimbali pamoja na waandishi wa habari katika ufunguzi rasmi wa ofisi zao jijini dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja miradi Stromme foundation, Doreen Matekele ameyasema haya;
“Kabla ya kufungua ofisi zetu hapa Tanzania tumekuwa tukifanya shughuli zetu kupitia ofisi za kanda, na kwa hapa tumekuwa tukifanya uratibu huu wa shughuli zetu Tanzania kupitia ofisi zetu za kanada zilizopo Kampala.
Siku ya Leo tuna furaha sana kuweza kufungua rasmi ofisi yetu ila hii haimaanishi kwamba ndio mara yetu ya kwanza kuanza kufanya kazi Tanzania. Tumefanya kazi Tanzania kwa muda wa miaka 20 iliopita kupitia wadau wetu mbalimbali katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Singida, Morogoro pamoja na Zanzibar.
Maana ya kufungua ofisi hapa Tanzania ni kutuwezesha kuwa karibu na wadau wetu ambao tunafanya nao kazi. Stromme foundation hatufanyi uwekezaji wa miradi hii moja kwa moja bali tunafanya kazi katika eneo husika katika kutimiza malengo yetu. Sisi tuko katika maeneo makuu mawili, elimu kwa maana ya kuboresha maeneo ya kujifunzia na kufundishia na kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma katika utowaji wa elimu Bora .
Pili ni kuboresha maisha yenye ustawi ya Wana jamii kupitia kuhakikisha kuna upatikanaji wa ajira kupitia shughuli mbalimbali zenye kipato, hii pia inafanyika katika miradi ya kilimo ambayo tunafanya katika mkoa wa singida na maeneo mbalimbali mengine.
Kwasasa utaratibu wa shughuli zetu hautokuwa tena inatokea ofisi za kanda ambayo ni Kampala bali itafanyika hapa Dar es salaam.
Tunashukuru serikali kwa kuweza kutoa uwezekano wa hao vijana kujipatia study hizi za kiufundi lakini pia lengo kuu ni ili hawa vijana waweze kujitengenezea kipato , tunafahamu katika ngazi ya halmashauri kuna ile mikopo wanayotoa kwa ajili ya vijana tungependa kutoa ari wale waliopata haya mafunzo wapewe Kipaombele ili waweze kufanyia kazi kwa haya maarifa waliopata kwasababu ni kupitia hio mikopo wanaweza kuboresha mitaji yao na kupitia hio mikopo wanaweza kufanya shughuli zao ili kujikwamua katika hali ya kiuchumi.