Rais wa Vladimir Putin wa Urusi amefanya mazungumzo na kiongozi wa kijeshi Mashariki ya Libya Khalifa Haftar jijini Moscow.
Vikosi vya Jenerali Haftar, vilitegemea pakubwa wapiganaji wa Urusi Wagner, ambao kwa sehemu kubwa bado wangali mashariki mwa Libya.
Msemaji wa Kremlin amesema viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali ya nchini Libya na eneo hilo la mashariki.
Vikosi vya Jenerali Haftar vinatawala eneo la mashariki ya Libya, wakati vile vya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa vikichukua uthibiti wa baadhi ya maeneo ya Magharibi.
Urusi kwa imeonekana kuendelea kutafuta mbinu za kutafuta ushawishi barani Afrika.
Huu ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu mwaka wa 2019 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Tripoli.
Mbabe huyo wa kivita wa mashariki ya Libya awali alikuwa amefanya mazungumzo na naibu waziri wa ulinzi wa Moscow Yunus-Bek Yevkurov wakati wa ziara yake.
Yevkurov amekuwa akizuru mashariki ya Libya katika miaka ya hivi karibuni, ziara ya hivi karibuni akiifanya tarehe 17 ya mwezi Septemba.