Naibu waziri wa nishati Judith Kapinga akiwa ziara mkoani Tabora ametembelea na kugagua mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha kupokea na kupoza umeme cha Uhuru kulichofikia asilimia 67 ambacho ujenzi wake unagharimu zaidi ya Bilioni 16 unaoendelea katika kijiji cha Vumilia wilayani Urambo.
Naibu Waziri Kapinga ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi huo utakaoongeza nguvu ya usambazaji wa umeme katika mikoa ya Kigoma,Karavi na Tabora ambapo amesisitiza mradi huo kumalizika kwa wakati ifikapo Julia 2024.
Aidha Naibu Waziri Kapinga amekuwa mkoani Tabora kwa ziara ya siku tatu kwaajili ya kuwasha huduma ya umeme katika vijiji mbalimbali vya mkoa huo kupita mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili ambayo gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 130 katika mkoa wa Tabora.