Kampuni ya Soft Bank ya nchini Japan imetengeneza Robot ambayo ina uwezo ya kuwasiliana na kusoma hisia za mwanadamu.
Robot hiyo iliyopewa jina la Pepper inadaiwa kuwa ina uwezo wa kufikiri kama mwanadamu na kufanya kile mtu atakachomwambia na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali kama binadamu.
Pepper mwenye urefu wa futi nne ni Robot ya kwanza yenye moyo ambapo ina uwezo kutambua sauti, ishara, maneno kupitia programu ya akili bandia iliyofungwa au ’emotional engine’.
Kampuni hiyo imesema kuwa watu wanaweza kuwasiliana na Robot hiyo kama wanavyowasiliana na marafiki na familia na linaweza kufanya shughuli nyingi.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.