Mbunge Esther Bulaya amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 20 zitakazoshiriki mashindano ya ‘Bulaya Cup 2023’ ambazo zimegharimu kiasi cha Tsh. milioni 20.
Akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za vijana kwa Bunda, Bulaya amewataka waamuzi wa mashindano kutenda haki kwa timu zote zitakazoshiriki huku akisisitiza kuwa yeye ni mpenda michezo na kuwa surprise zake bado zitaendelea.
Bulaya amekabidhi jezi na mipira kwa timu zote 20, ambazo zitashiriki katika michuano ya ‘Bulaya Cup 2023’ itakayodumu ndani ya mwezi mmoja akiahidi kutoa zawadi nono kwa mshindi wa kwanza hadi watatu.