Mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea ya wanawake, Lauren James, amefichua kwamba anahitaji kupata chakula cha jioni na mwimbaji wa Nigeria aliyeshinda tuzo ya Grammy, Damini Ogulu, almaarufu Burna Boy.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 22 alifichua hayo alipokuwa akitaja orodha ya watu watatu ambao angewaalika kwa chakula cha jioni katika mahojiano ya hivi majuzi na Sky News.
Mtangazaji: “Watu watatu ambao ungewaalika kwa chakula cha jioni?”
Lauren: “Wewe mtangazaji, Kevin Hart kwakuwa ni mcheshi sana na mtu wa tatu pengine angekuwa mwimbaji na pengine ningesema Burna Boy.”