Donald Trump anatazamiwa kujitokeza kwa kushtukiza katika siku ya kwanza ya kesi yake ya ulaghai inayoanza leo New York.
Rais huyo wa zamani, ambaye ndiye anayependekezwa zaidi kuwa mgombea urais wa chama cha Republican mwaka ujao, ndiye mshtakiwa mkuu katika kesi ya madai inayoanza leo katika chumba cha mahakama kusini mwa Manhattan.
Trump, pamoja na watu kadhaa wa familia yake na washirika wengine, anatuhumiwa kuongeza thamani ya milki ya Trump kwa mabilioni ya dola ili kupata mikopo katika kesi iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James.
Jumanne wiki iliyopita, uamuzi wa ajabu wa kabla ya kesi uliotolewa na Jaji Arthur Engoron, ulianzisha matarajio ya Trump kupoteza leseni yake ya biashara ya New York ambayo inaweza kumlazimisha kuuza mali yake yote ya New York ikiwa ni pamoja na jengo la kifahari la Trump Tower kwenye 5th Avenue.
Trump alikuwa anatarajiwa kutohudhuria kesi hii isipokuwa kulazimishwa kutoa ushahidi.
Hata hivyo, nyaraka za mahakama katika kesi tofauti, iliyochapishwa mwishoni mwa wiki iliyopita, zinadokeza uwezekano wa mzozo kati ya Jaji Engoron ambaye amemtaja kuwa ‘aliyechanganyikiwa’.
Trump alikuwa amefikishwa mahakamani huko Florida katika kesi aliyoleta kumshtaki wakili wake wa zamani, Michael Cohen.
Hata hivyo ametaka kuchelewesha kesi hiyo ili ajitokeze mwenyewe kwenye kesi ya New York badala yake