Takwimu zilizovuja zinaonyesha matumizi ya ulinzi ya Urusi yanaweza kuongezeka kwa asilimia 30: Uingereza
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, katika taarifa yake ya hivi punde kuhusu vita vya Ukraine, inasema matumizi ya Urusi katika ulinzi yanatarajiwa kuongezeka hadi takriban asilimia 30 ya jumla ya matumizi ya umma mwaka ujao, kulingana na nyaraka zilizovuja kutoka Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Wizara inapendekeza bajeti ya ulinzi sawa na karibu asilimia 6 ya Pato la Taifa la nchi na ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na 2023, sasisho linasema, na kuongeza, takwimu hizi zinaonyesha kuwa Urusi inajiandaa kwa miaka zaidi ya mapigano nchini Ukraine.
Haya yanajiri wakati msaada wa EU kwa Ukraine ‘sio tu unaendelea, lakini unaongezeka’mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borrell alisema Jumapili.
“Msaada wetu kwa Ukraine sio tu unaendelea, lakini unaongezeka, au angalau kwa wakati huu, kifungu kilicho kwenye meza kinaonyesha kwamba tunataka kuendelea kuiongeza,” Borrell alisema katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mkutano ambao haujawahi kufanywa na mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo. mjini Kyiv uliopangwa kufanyika Jumatatu.
Usaidizi wa kijeshi wa Brussels kwa Ukraine umefikia euro bilioni 25 (dola bilioni 26.4), Borrell alisema, akiongeza kuwa kwa ujumla, msaada wa kijeshi, kiraia na kibinadamu umefikia euro bilioni 85 ($ 89.8 bilioni).
Kiasi kama hicho ni “cha juu zaidi ulimwenguni, na tunajivunia na tunajua jinsi ilivyo muhimu”, alisema.