Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita Frank Chang”awa amesema wamejipanga kuhakikisha wananchi wa Mji wa Geita wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 100 ili kukuza kasi ya Uchumi ndani ya Mji wa Geita.
Akizungumza hayo na wandishi wa habari Mjini Geita katika kuhitimisha Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini Mhandisi Chang”awa amesema wamepanga Mipango ya Mda mrefu pamoja na Mipango ya Mda mfupi katika kuhakikisha Mji wa Geita unaondokana na Tatizo la Maji Kwa wananchi.
Chang”awa amesema kwa sasa wanamiradi mbalimbali ya Mpango wa Mda Mfupi katika kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 75 ambapo maji yanatoka kwa Masaa 14 kwa wastani badala ya Masaa 20 ambapo amebainisha kuna Maeneo mengi wanapata maji kwa Mgao.
“Kwa sasa tuna Miradi mbalimbali ya Mpango wa Mda Mfupi ya kuongeza upatikanaji wa Maji tuko Asilimia 75 na huduma ya Maji inatoka kwa Masaa 14 kwa wastani Badala ya Masaa 20 Maan yake kuna maeneo mengi yanapata maji kwa Mgao, ” Mhandisi Chang”awa.
Mhandisi Changawa amesema katika kufikia wananchi wapate maji tayari wana mradi wa kutanua chujio Nyankanga ambao una thamani ya Bilioni 1.1 ambapo kwasasa umefikia asilimia 90 kupitia Mradi huo wa utanuwaji ambacho ni moja ya vyanzo vinne vinavyotumika katika Mji wa Geita kupeleka Maji Mjini.
Mhandisi Chang”awa amesema kupitia Chanzo cha Bwawa na Ziwa kina uwezo wa kushiriki katika Chujio moja ambapo kina uwezo wa kuzalisha lita 2 kwa saa ambapo kutanuliwa kwake litakuwa likizarisha lita laki 3 na 50 kwa saa kwa maana hiyo tutakuwa na wastani wa kupata lita Milioni 7 kwa siku Badala ya Milioni 4 ambapo mradi huo wanatarajia ukamilike mwezi wa 10 .
“Kupitia chanzo cha Bwawa la ziwa kina share chujio Moja lina uwezo wa kuzalisha lita laki 2 kwa saa tunaenda kulitanua linaenda kuzarisha lita laki 3 na 50 kwa saa kwa maana hiyo tutakuwa na wastani wa kupata maji lita Milioni 7 kwa siku Badala ya Lita milioni 4 ,” Mhandisi Chang”awa.