Shambulio hili limetajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo tangu jeshi kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai.
Katika taarifa iliyotolewa kwa njia ya televisheni, mamlaka nchini Niger imesema vikosi vyake vilishambuliwa na zaidi ya wanajihadi 100 waliokuwa wamejihami kwa bunduki na vilipuzi.
Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kuwaomboleza maofisa hao waliouawa wakilinda taifa lao.
Mashambulio yanayotekelezwa na makundi ya kijihadi dhidi ya vikosi vya usalama yamekuwa yakiongezeka tangu jeshi kuchukua madaraka.
Licha ya mashambulio hayo, serikali ya kijeshi kwa upande wake imeahidi kupambana na kumaliza makundi hayo ya watu wenye silaha.