Wakati mjadala unafanyika nchini Marekani juu ya kiwango cha misaada ya kuendelea kutuma kwa Ukraine, ni vyema kukumbuka jinsi imekuwa muhimu kwa juhudi za vita vya nchi hiyo.
Kufikia Julai 31, Marekani imetoa msaada mkubwa zaidi wa kijeshi kuliko mshirika yeyote, £36.6bn – zaidi ya wafadhili 10 wakuu waliofuata kwa pamoja, kulingana na Taasisi ya Kiel ya Uchumi wa Dunia.
Bila msaada wa kijeshi kutoka kwa Marekani, wanajeshi wa Ukraine wangekosa risasi kwa ajili ya operesheni za ardhini na vifaa vinavyotumika kusitisha mashambulizi ya Urusi, wataalam waliambia AFP.
“Jeshi la Ukraine lingedhoofika na hatimaye pengine kuanguka”, ingawa “linaweza kushikilia tu kujihami,” Mark Cancian, mshauri mkuu katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, alisema.
Lakini huenda Moscow isingeweza kuchukua fursa ya hali kama hiyo, kutokana na uchovu wa jeshi lake yenyewe, aliiambia AFP.
Kuondoa teknolojia ya Marekani kutoka kwa ulinzi wa anga pia kunaweza kuharibu mfumo mzima kwa sababu umeunganishwa sana, kulingana na James Black, mkurugenzi msaidizi wa kikundi cha utafiti wa ulinzi na usalama katika RAND Europe.
Alisema itachukua “miaka na juhudi za miongo kadhaa” kwa juhudi za kujaza pengo la misaada ya kijeshi lililoachwa na Merika.