Zaidi ya wahudumu 100 wa afya walikufa nchini Libya baada ya mafuriko mwezi uliopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema.
Ni miongoni mwa watu 4,000 ambao hadi sasa wamethibitishwa kufariki, ilisema, na kuongeza kuwa zaidi ya 8,500 bado hawajapatikana.
“Madaktari, wauguzi na wahudumu hawa 101 waliopoteza maisha sio tu kwamba wanakumbukwa na familia zao na wapendwa wao; jamii nzima imeathiriwa na kuondoka kwao na hakika sekta ya afya mashariki mwa Libya na kwingineko itaathirika pakubwa, alisema Mwakilishi wa WHO nchini Libya Dk Ahmed Zouiten katika kuwaenzi wahudumu wa afya.
Maafa hayo yametokea baada ya mabwawa mawili ambayo hayakutunzwa vizuri huku kukiwa na mzozo wa miaka mingi nchini kupasuka chini ya shinikizo la mvua kali iliyotokana na kimbunga Daniel.
Vitongoji vyote vilitoweka baharini huku maji yakipiga mashariki mwa Libya, ukiwemo mji ulioathirika zaidi wa Derna