Uongozi wa Kijiji cha Olevolosi kilichopo Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha umepitisha sheria ndogo ikiwemo inayopiga marufuku Watu kunywa pombe saa za kazi na atakayekwenda kinyume atalipa faini isiyopungua Tsh. Elfu 50.
Akisoma sheria hizo ndogo mbele ya Wananchi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kimnyak, Joshua Mollel amesema “Ni kosa kulewa au kunywa pombe saa za kazi , adhabu yake faini isiyopungua elfu 50, ukikamtwa tunakupa akaunti namba ulipie, ukishindwa kamati husika itafanya kazi yake”
“Ni kosa pia kuuza pombe haramu ya gongo, kosa kuuza pombe haramu ya moshi, na kosa kuuza bangi, adhabu yake ni kufikishwa Mahakamni, ni kosa kuuza pombe saa za kazi adhabu yake Tsh. elfu 50”
Mwenyekiti wa Kijiji cha Olevolos, Emmanuel Ngailuva amesema lengo la sheria hizo ni kukabiliana na mmomonyoko wa maadili ambapo Wazee wa Kijiji wamekubali uwepo wa sheria hizo ambazo Wananchi wamezipitisha kwa pamoja na kukubali zianze kutumika.