Idadi ya wakimbizi nchini Uganda wanatatizika kunusurika kufuatia kupunguzwa kwa misaada ya kibinadamu, kulingana na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa.
Likikabiliwa na upungufu wa ufadhili wa zaidi ya asilimia 60 kwa mahitaji yake ya kimataifa, wakala wa chakula wa Umoja wa Mataifa ulilazimika kupunguza mgao wake wa chakula nchini Uganda kutoka asilimia 70 hadi 30 mwezi Julai mwaka huu na kuwapa kipaumbele wale walio hatarini zaidi.
Shirika hilo linasema kupunguzwa zaidi kunawezekana kuja.
Huku kukiwa na uwezekano wa upungufu zaidi, kuweka chakula mezani kumekuwa vita vya kila siku kwa wakimbizi wengi wa nchi hiyo.
Uganda inawahifadhi wakimbizi wengi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika, ikiwa na takriban wakimbizi milioni 1.5 na waomba hifadhi 32,000 wanaoishi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwaka 2022.
Huku wakimbizi wakiendelea kuwasili, wengi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini, mgao uliopunguzwa wa chakula unahatarisha maisha.
Wakimbizi wengi wamegeukia biashara ndogondogo huku wengine wakiamua kuuza vitu vyao, huku wengine wakilazimika kujihusisha na uhalifu ili kujinusuru.
“Tunaona baadhi yao wakiamua kuuza mali zao za nyumbani. Wana mbuzi au kikombe au hata redio au simu, na wanauza hivyo,” alisema Santo Asiimwe, mfanyakazi wa WFP katika makazi ya Nakivale karibu na mpaka na. Tanzania.
Hadi asilimia 70 ya wakimbizi huko Nakivale ni akina mama ambao wanatamani sana kutafuta njia za kuwatunza watoto wao.