Ni Kocha wa Young Africans, Miguel Gamondi ambae leo Octoba 3, 2023 amekutana na vyombo vya habari kuzungumza mchezo wakaocheza dhidi ya Ihefu Mkoani Mbeya.
“Tunashukuru tumefika salama Mbeya, hatukuweza kupata muda mzuri wa kujiandaa kama mnavyojua tumetoka kucheza mchezo wa Kimataifa Jumamosi lakini tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu na tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu”- Miguel Gamondi
“Wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali yao iko juu, kuna baadhi ya wachezaji wana majeraha lakini tutajua kwenye mazoezi ya mwisho leo jioni ni wachezaji wapi watakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho”- Miguel Gamondi
“Tunafahamu kwamba ni mwanzo wa ligi na kila timu iko kwenye nafasi nzuri na kujaribu kufanya vizuri zaidi inapokutana na bingwa mtetezi, ni sisi sasa kuhakikisha tunaendelea kucheza kwa kiwango cha juu na nina imani tutaendelea kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho”- Miguel Gamondi