Watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC) wameitaka mamlaka pamoja na taasisi za huduma hizo kuzingatia taratibu na haki ya wateja wanapotoa huduma.
Akizungumza na wandishi wa habari Afisa tawala msaidizi kutoka EWURA, Wadi Omari amesema mbali na kutoa huduma ana wajibu wa kutambua mteja wake ana haki ya kupewa huduma sahihi, stahiki na kwa wakati pindi anapolipia na inapotokea dharura afahamishwe.
Amesema mtu anapolipia huduma ya umeme anapaswa ndani ya siku 30 za kazi awe ameunganishiwa, na endapo kuna changamoto atahitaji ajulishwe .
“Huduma hizi (maji na nishati) ni huduma kiritimba, kwa maana hazina mbadala, kwa maana kwamba binadamu anapohitaji maji anahitaji maji, anapohitaji umeme anahitaji umeme.” Afisa Tawala Wadi.
Amesisitiza kuwa kanuni ya utoaji huduma inaelekeza indapo mtoa huduma atachewesha kuunganisha huduma ya maji na umeme atapaswa kumfidia mteja wake kwa pesa taslimu ama kihuduma.
“Kwa kipindi hiki katika siku ambazo tupo hapa, tumekusanya malalamiko zaidi ya 15, ambapo malalamiko mengi yamekuwa yakitokea kwenye sekta ya maji, umeme pamoja na mafuta Tuna malalamiko ambayo yanatokana na kuchelewa kuunganishwa huduma, kwenye sekta ya umeme kwa mfano tangu kipindi kile watu wanalipa Sh 27,000/= tunao watu mpaka sasa hawajaunganishwa, ” Afisa Tawala EWURA CC.
Ameahidi EWURA CCC inaendelea kuwasiliana na Mamlaka husika ili kutatua Malalamiko huku akiwataka watanzania kufuata taratibu za utoajia malalamiko badala ya kubaki na manung’uniko nyumbani.