Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amezitaka taasisi za serikali na kutumia vizuri fedha zinazotolewa na wahisani ili sababu za kutoa fedha hizo ionekane.
Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo wakati akizindua gari linalotumia nishati ya gesi inayozalishwa kwa taka ngumu(BIO GAS) ikiwa ni ishara ya kusherehekea miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden katika Nishati.
Waziri Dkt. Biteko amesema serikali ya Sweden imeisaidia Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 142 kupitia Wakala wa Nishati Vijijni REA kwaajili ya mradi wa umeme ujazilizi katika vitongoji 1328 vyenye wateja Zaidi ya laki moja (100,000),pia shilingi bilioni 52 kwaajili ya kuunganisha umeme katika vijiji 151
Akizungumzia uzalishaji wa gesi kupitia taka ngumu Biteko amesema “taka tunazozizalisha hapa nchini na sisi tuzifanye kuwa nishati ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi kwasababu tutapunguza kiasi cha uchafuzi na tutazifanya hizo taka ziwe na maana Zaidi”