“Mtwara walikuwa na changamoto ya Miundombinu chakavu. Miundombinu iliyokuwepo Mtwara ilikuwa chakavu sana. Sasa Rais ametoa Bilioni 20 sasa hivi tunatoa miundombinu yote chakavu na kuongeza uzalishaji. Tunavyoongea Mkandarasi yuko saiti na kukamilika kwa mradi huo inamaanisha eneo lote la Mtwara hakutakuwa na miundombinu chakavu” – Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso
“Mtwara walikuwa na mahitaji yao. Walihitaji kupata chujio maana ni haki ya mwananchi kupata maji lakini yawe safi, salama na yenye kuzingatia ubora kwahiyo walihitaji chujio ili wapate maji yenye ubora. Tunamshukuru Mhe. Rais alitupa Bilioni 3.4 na ule mradi tuliujenga na wataalamu wetu wenyewe. Kama ungejengwa na Mkandarasi ulitakiwa kujengwa kwa Bilioni 5 lakini tuliwatia moyo wataalamu wetu hapa nyumbani na kuwaambia kwamba kuna kazi tunatakiwa kufanya sisi wenyewe na niwapongeze sana wataalamu wa Mtwara kwa kazi kubwa waliyoifanya” – Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso