Ni Octoba 5, 2023 ambapo Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Meja Jenerali, Francis Mbindi wamemtembelea na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wetu, Abdulmajid Nsekela ofisini kwake, Makao Makuu ya Benki jijini Dar es Salaam.
Safari hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Kimataifa la Michezo ya Kijeshi Duniani (79th CISM General Assembly & Congress) utakaofanyika nchini kuanzia Mei 12 mpaka 19, 2024.
Benki yetu inashirikiana na JWTZ kuhakikisha maandalizi ya Mkutano huo yanafanyika kikamilifu na tukiwa wadau wakubwa wa sekta binafsi na taasisi za Serikali tunaamini kuwa Mkutano huo utaleta fursa mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa Nchi yetu ikiwamo Utalii, Biashara na Michezo.