Ripoti ya mwisho kuhusu chanzo cha ajali ya ndege iliyomuua Yevgeny Prigozhin bado haijatolewa, Ikulu ya Kremlin imesema.
Kiongozi huyo wa kundi la Wagner alifariki miezi miwili kamili baada ya kuongoza maasi dhidi ya wakuu wa jeshi la Urusi mjini Moscow.
Watu wengine tisa pia waliuawa katika ajali hiyo.
Waangalizi wengi, na baadhi ya wafuasi wa mkuu wa mamluki, wamesema serikali ya Urusi ilihusika.
Baadhi wamependekeza Vladimir Putin huenda alitaka kuiangusha ndege ili kulipiza kisasi kwa uasi huo.
Rais wa Marekani Joe Biden ni miongoni mwa wanaoamini kuwa kiongozi huyo wa Urusi alihusika.
Jana, rais Putin alisema vipande vya maguruneti ya mkono vilipatikana katika miili ya waathiriwa.