Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu ameridhia kufutwa kwa hati za umiliki wa ardhi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Katavi (KUA) na kuwaacha Wananchi wa kaya zaidi ya 400 ambayo inaishi maeneo hayo na kupimiwa ardhi hiyo.
Akiongea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ametoa maelekezo kwa Kamishna wa Ardhi nchini kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo atoe ilani ya kufanya marekebisho ya daftari ya usajili wa hati ndani ya siku 30 ambayo inaisha November 07, 2023 na kufuta hati hizo za kwanza.
“Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Katavi na Afisa Mipango Miji wa Mkoa anzeni mchakato wa upimaji wa maeneo yale, siku kumi kuanzia November 07,2023 baada ya Bunge nitakuja hapa kukabidhi hati kwa Wananchi wale wakae kwa raha mustarehe”
Mgogoro huo umedumu toka mwaka 2012 na Wananchi wa Katavi wamemshukuru sana Silaa kwa kuumaliza rasmi.