Mashabiki wataweza kununua jezi ya mlinda mlango wa AC Milan huku jina la Olivier Giroud likiwa limechapishwa mgongoni, klabu hiyo ya Serie A ilisema baada ya mshambuliaji huyo kufunga goli katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Genoa Jumamosi.
Kipa wa Milan Mike Maignan alionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa dakika za lala salama na Giroud akachukua nafasi yake, na kuokoa vyema kumnyima George Puscas kabla tu ya kipenga cha mwisho.
Milan pia ilimuongeza Giroud kwenye orodha ya makipa wa kikosi cha kwanza kwenye tovuti yake.
“Jana usiku Olivier Giroud alikua sehemu ya historia ya Milan kwa kulinda kwa ujasiri lango la AC Milan katika dakika za mwisho za mechi ya Rossoneri dhidi ya Genoa,” Milan ilisema katika taarifa.
“Klabu imeamua kuheshimu uchezaji wake katika safu yake ya mwisho ya ulinzi kwa kumuweka katika orodha ya makipa. Zaidi ya hayo, mashabiki sasa wanaweza kununua jezi ya golikipa na kuigeuza kukufaa kwa ‘Giroud 9’.”
Jezi ya golikipa wa nyumbani katika duka rasmi la Milan itauzwa Jumatatu.